Dar es Salaam +255 712 345 678
Msaada Swahili
Jinsi Inavyofanya Kazi — Konektika

Konektika Inavyofanya Kazi

Tumeunda mfumo rahisi, wa haraka na salama kukuunganisha na wataalamu au kupata wateja ndani ya sekunde chache.

Msaidizi wa AI (AI Assistant)

Hujui kategoria sahihi? Elezea tatizo lako kwa lugha ya kawaida (mf. "sink linavuja") na AI yetu itakupeleka moja kwa moja kwa Fundi Bomba sahihi.

Kitufe cha Dharura (KONEKTIKA NOW)

Kwa matatizo ya dharura kama shoti ya umeme au bomba kupasuka, tumia kitufe cha dharura kuunganishwa na mtaalamu aliye karibu zaidi kwa haraka.

Safari Yako Ndani ya Konektika

Kwa Mteja (Customer)

1. Tafuta Huduma

Fungua mfumo, chagua kategoria, au tumia Konektika AI kuelezea tatizo lako kwa urahisi.

2. Chagua Mtaalamu

Mfumo utakuonyesha wataalamu walio karibu nawe (GPS Based), wenye rating nzuri, na wanaopatikana.

3. Omba Huduma

Chagua mtoa huduma, tuma maombi ya kazi, na pokea quotation (makadirio ya bei) ya haraka.

4. Fuatilia na Lipa

Baada ya kazi kukamilika, lipa kwa usalama kupitia mifumo ya simu (M-Pesa, Tigo Pesa) ndani ya mfumo.

5. Kadiria Huduma

Toa rating na review kusaidia wateja wengine kupata huduma bora kutoka kwa mtaalamu huyo.

Kwa Mtoa Huduma (Provider)

1. Jisajili na Uthibitishwe

Jaza wasifu wako, pakia kitambulisho na vyeti vya ujuzi ili kupata hadhi ya Verified Provider.

2. Pokea Maombi

Utapata notification ya kazi mpya zinazoingia katika maeneo yako ya kazi kwa wakati sahihi.

3. Tuma Quotation

Angalia maelezo ya kazi aliyotuma mteja, kisha mtumie bei yako ya kutoa huduma husika.

4. Toa Huduma

Baada ya mteja kukubali ofa yako, fanya kazi yako kwa uaminifu na ubora wa hali ya juu.

5. Pokea Malipo

Pesa zako zitaingia kwenye akaunti yako salama baada ya kazi kukamilika na kuthibitishwa.

Upo Tayari Kuanza?

Jiunge na Konektika leo. Tafuta mtaalamu wa kutatua tatizo lako, au sajili ujuzi wako uanze kupata wateja mara moja.

👋 Pata Msahada hapa
Usaidizi wa Ramani