Kuhusu Konektika
Tunabadilisha namna huduma za kila siku zinavyopatikana Tanzania na Afrika Mashariki kupitia teknolojia ya kisasa na ya kuaminika.
Sisi Ni Nani
Konektika ni jukwaa bunifu la kidijitali linaloleta mapinduzi katika upatikanaji wa huduma za kila siku kwa kuwaunganisha watu binafsi, kaya, na wafanyabiashara moja kwa moja na watoa huduma au mafundi stadi waliothibitishwa. Kupitia mfumo wetu unaopatikana kupitia programu za simu za mkononi na mtandao wa intaneti (Mobile App na Web Platform), tunarahisisha namna huduma zinavyotafutwa, kuombwa, na kutolewa kwa haraka, usalama, na uhakika.
Dira Yetu
Kuwa jukwaa kubwa na la kuaminika zaidi nchini Tanzania na Afrika Mashariki la kuunganisha wateja na wataalamu wa huduma kwa ufanisi wa hali ya juu na teknolojia ya kisasa.
Dhamira Yetu
Kutoa suluhisho la haraka la kidijitali ambalo linaondoa changamoto ya kupata wataalamu wa kuaminika wakati wa dharura au mahitaji ya kawaida, huku tukiwakunjulia wigo mpana watoa huduma kukuza biashara zao na kupata wateja wapya kwa urahisi.
Tatizo Tunalolitatua
Kupata fundi au mtaalamu mwenye uaminifu, kujua ubora wa kazi kabla ya kuajiri, na kupata msaada wa haraka wakati wa dharura imekuwa ni changamoto kubwa kwa jamii nyingi. Vilevile, watoa huduma wengi stadi wanakosa njia rahisi ya kufika kwa wateja wengi. Konektika inasimama kama daraja linaloaminika linalounganisha pande zote mbili kwa mfumo wa uwazi, viwango vya ubora (ratings and reviews), na malipo salama.
Kwa Nini Uchague Konektika?
Sababu zinazotufanya kuwa chaguo nambari moja la huduma bora
Wataalamu Waliothibitishwa
Tunahakikisha usalama wako kupitia mchakato thabiti wa uhakiki wa vitambulisho na uwezo wa wataalamu wetu (Verified Providers).
Teknologia ya GPS
Mfumo wetu unatumia teknolojia ya eneo lako kukutanisha na mtaalamu aliye karibu zaidi na anayepatikana kwa wakati huo.
Msaidizi wa AI
Unaweza kuelezea tatizo lako kwa lugha ya kawaida kabisa, na AI yetu itakusaidia kutambua huduma na kukupeleka kwa mtaalamu sahihi.
Huduma za Dharura
Suluhisho la haraka la kukutanisha na wataalamu pindi zinapotokea dharura za ghafla kama vile shida za umeme, mabomba, au gari.
"Tafuta huduma. Unganishwa na mtaalamu. Pata suluhisho."
Tunataka kufanya upatikanaji wa huduma zote uwe rahisi kama kubonyeza kitufe kimoja. Jiunge nasi leo uwe mteja au mtoa huduma.